NSSF YACHANGIA VIFAA VYA ICU HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.

Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Jumanne Mbepo (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 20
Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Marina
Njelekela kwa ajili ya kununulia vifaa vya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. 
Kutoka kushoto ni Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Devota Ikandilo, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk John Kimario, Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Marina Njelekela na Ofisa Uhusiano wa NSSF, Jumanne Mbepo wakkwa katika picha ya pamoja baada ya NSSF kukabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 20 kwa ajili ya kununulia vifaa vya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. 
Na Mwandishi Wetu
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umechangia kiasi cha shilingi
milioni 20 kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Msaada huo utatumika
kununulia vifaa kwa ajili ya chumba cha Wagonjwa mahututi (ICU).
 Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili.

Dk. Marina Njelekela aliishukuru NSSF kwa msaada huo na kuongeza kuwa
msaada huo utaenda kuokoa maisha ya watanzania wengi.
  Pia aliwashauri NSSF kushiriki kwenye clinic Maalumu ya upimaji wa Kansa ya
Matiti kwa kina mama ambalo hufanyika hospitalini hapo..


Nae Mwakilishi wa NSSF, Jumanne Mbepo alisema kua mchango uliotolewa na NSSF
kwa hospitali hiyo hautoshi kununua vifaa vyote na kuomba Taasisi
nyingine ziichangie Hospitali hiyo ili kuweza kuokoa maisha ya
Watanzania wengi zaidi..

NSSF imekuwa ikitoa huduma ya bima ya Afya kwa wanachama wake ijulikanayo kama SHIB , Hospitali ya muhimbili ni mojawapo ya watoa huduma wa bima hiyo.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment