
..............................................................................
Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira imeendelea na ukaguzi katika Migodi ya dhahabu kufahamu utekelezaji wa Sheri a ya Mazingira. Katika Mgodi wa Bulyanhulu Kamati iliangalia jinsi maji yenye kemikali yanavyohifadhiwa na udhibiti wa taka za plastiki mgodini hapo. Migodi iliyotembelewa mpaka sasa ni Mgodi wa North Mara, Geita na Bulyanhulu. Hii leo Kamati hii itaendelea na ziara yake katika mgodi wa Buzwagi.
Pichani ni taka za plastiki zilizohifadhiwa vizuri kwa ajili ya urejelezwaji katika Mgodi wa Bulyanhulu.
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu wakati wa ukaguzi katika Mgodi huo kuona utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu mara baada ya ukaguzi katika Mgodi huo kuona utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.
0 comments :
Post a Comment