Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mojawapo ya nyumba iliyokuwa ya mfano wakati wa ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu wakizishuhudia mashine za kufyatulia matofali aina ya Hydraform ambazo zitagawanywa kwenye wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma ili kuwezesha vikundi vilivyoanzishwa vya ujenzi vya vijana kuendelea na mafunzo .
................................................................................................................................
Rais Kikwete amerejea kauli yake aliyoitoa Kasera, Mkinga Tanga kwamba Halmashauri zizipatie taasisi zingine zinazojishughulisha na uendelezaji miliki kama NSSF, PPF, GEPF, PSPF, LAPF na kadhalika maeneo kwa masharti ili ziweze kujenga.
Rais Kikwete aliambiwa kuwa katika eneo hilo la Mkuzo, shirika hilo limejenga kiasi cha nyumba 18 za kuuza na zimejengwa kwa gharama ya sh. milioni 676.
Rais Kikwete pia ameambiwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge Shambwe kuwa nyumba hizo zimejengwa katika kutekeleza kaulimbiu ya NHC ya “Nyumba yangu, Maisha yangu” ambayo mpaka sasa inatekelezwa katika mikoa 14. Ujenzi wa nyumba hizo ulianza Januari mwaka jana na unakamilika mwezi ujao, Agosti, 2014.
Nyumba hizo, ameambiwa Rais Kikwete, kuwa zitauzwa kwa gharama ya kati ya sh. milioni 33 na 44 bila kodi ya VAT lakini ambayo inaongezeka na kuwa kati ya milioni 44 na 52 kwa kutegemea ukubwa wa nyumba – kuanzia ya vyumba viwili hadi nyumba vitatu. Rais Kikwete anaendelea na ziara yake mkoani humo.
Mkuzo Housing Estate ni mradi wa nyumba 18 zilizopangwa kwa kuzingatia vigezo vya miji ya kisasa yenye huduma za msingi zikiwemo Zahanati , shule ya Chekechea , maduka , sehemu za shughuli mbalimbali za jumuiya, barabara pana inayotoa fursa kwa watembea kwa miguu na baiskeli kuwa huru vile vile imezingatia nafasi za miundombinu kama vile mitaro na umeme.
Kila nyumba inajitegemea ikiwa na eneo kubwa kwaajili ya matumizi binafsi ya wakazi pamoja na eneo la maegesho ya magari hadi matatu.
Mkuzo Housing estate ina nyumba za aina mbili, nyumba za vyumba vitatuna nyumba za vyumba viwili . Nyumba za vyumba vitatu zin aukubwa wa mita za mraba 85 kwa zile zenye jiko la nje na mita 70 zenye jiko la ndani. Huku nyumba ya vyumba viwili ikiwa na mita za mraba 56. Zinauzwa kati ya Sh 33 milioni bila VAT na 44 milioni.
Habari kupitia Full Shangwa blog.
0 comments :
Post a Comment