SEREKALI YASITISHA VIBALI VYA VIWANDA VYA KUNUNUA KUNI.



Na Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI imesitisha vibali vyote vilivyotolewa vya kununua kuni na magogo kwa ajili ya nishati ya  kuendesha viwanda mbalimbali nchini  na badala yake imevitaka ndani ya muda wa miezi mitatu (3) viwe vinatumia teknolojia ya makaa ya mawe, umeme, na gesi kwa ajili ya kuendeshaji wa viwanda hivyo.

Agizo hilo limetolewa  na Waziri wa Nchi  Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira  Dkt Binilith Mahenge baada ya kufanya ziara kiwanda cha kufuma nguo cha Sunflag Tanzania ltd, kilichopo eneo la Themi jijini Arusha na kushutushwa na shehena kubwa  ya magogo  yaliyorundikwa katika kiwanda cha Sunflug ambayo kiwanda hutumia  kwa ajili ya nishati
 "Hali hii inatisha sana katika  suala la mazingira na kamwe serikali halitalivumilia kwa kiwanda kama hiki  kukata miti kwa kiwango kikubwa hicho na huu ni uharibifu mkubwa wa mazingira "alisema waziri mahenge. 

Kufuatia hali hiyo Waziri Dkt Mahenge  amefuta vibali vyote  vilivyotolewa kwa kiwanda hicho kwa ajili ya kununua kuni kwa ajili ya Nishati kufuatia   hali hiyo ya kutisha ya kuwepo na shehena  ya magogo Serikali imeuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuacha mara moja matumizi ya  nishati ya magogo kuanzia sasa, na imetoa muda wa miezi mitatu kiwanda kiwe kimeaanza kutumia nishati ya gesi, umeme, na makaa ya mawe. 

Ameuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha kinawalipa walinzi watakaowekwa na serikali ngazi ya mkoa ili kuzuia uingizwaji wa magogo na kuni kiwandani hapo kwa ajili ya nishati.

Katika hatua nyingine waziri amekitoza faini ya shilingi milioni 80 kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira, na kukiagiza kushirikiana na mkoa pamoja na baraza la taifa la mazingira kanda ya kaskazini kutafuta eneo litakalopandwa miti milioni 7. 

Waziri amezitaja sababu mbali mbali zinazosababisha afrika kuendelea kuwa maskini kuwa ni pamoja na kuwa tuko nyuma katika matumizi ya sayansi na teknolojia, hatuna elimu kubwa ya kukabiliana  na majanga mbalimbali ikiwemo njaa na mafuriko yanayoharibu miundo mbinu ,kiwango kikubwa cha uharibifu wa mazingira ,mabadiliko ya tabia nchi, hivyo mkazo zaidi unawekwa kupunguza matumizi ya kuni na badala yake kusisiotiza matumizi ya sayansi na teknolojia.

Waziri huyo wa Mazingira ambaye pia ni mbunge wa Makete mkoani Njombe amesisitiza kuwa matumizi ya nishati  ya magogo katika uendeshaji  maboila katika kiwanda umepitwa na wakati kutokana na mabadiliko ya Teknolojia Hali hii imeshutua sana waziri Mahenge baada ya kuona  shehena kubwa ya magogo hayo ambayo inaaminika  yamevunwa kwa kipindi cha miaka mingi ambapo kila siku  kiwanda hicho hutumia tani zaidi ya 1,500 za magogo kama nishati.

 Akizungumza  wakati wa ziara ya kiwanda hicho Mkurugenzi  Mkuu wa baraza la taifa la mazingira katika ofisi ya Makamu wa Rais  Eng.Boneventura Baya amesema hali hii ni mbaya  na haikubaliki kabisa  imechangia kwa kiwango kikubwa katika uharibifu wa mazingira. 

Amemwagiza Mwanasheria wa Baraza la taifa la mazingira, Machale  Heche  kuchukua hatua za haraka kuanzia leo  kusimamisha uingizaji wa magogo katika kiwanda hicho na kusisitiza kuwa kuanzia jana hakuna mzigo au shehena ya aina yeyote ya kuni na magogo itakayoingizwa kiwandani hapo na oda zote zilizokuwa zimetolewa na kiwanda hicho za ununuzi wa kuni na magogo zimesimamishwa. 

Mhandisi Baya alisema kiwanda hicho kimekuwa kikivuna miti ya asili na ile ya kupanda hali ambao imechangia uharibifu mkubwa wa mazingira. 
Amesema magogo yamevunwa kwa zaidi ya miaka saba hivyo ameonya kwamba tuogope kuchezea suala la mazingira.

Kwa upande wake Mwanasheria katika baraza la Mazingira la taifa Manchale Heche  amesema kutokana na  shehena kubwa ya miti iliyovunwa na kiwanda hicho uongozi wa kiwanda hicho unapaswa kupanda zaidi ya miti milioni saba ili kufidia uharibifu huo.Amesisitiza kwamba kiwanda hiki kimechangia  mabadiliko makubwa katika mfumo wa  hali ya hewa.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment