Lekeshia Henry-Richards, 28, aliiba sahihi za wateja 150 waliokuwa wakitumia huduma binafsi katika jiji la London.
Taarifa hizo zilitumika kuwaibia wateja ambapo wateja kadhaa wameibiwa kupitia kundi hilo la kihalifu kabla ya ishu nzima kugundulika April mwaka huu na mwanamke huyo kufikishwa mahakamani.
Mwanamke huyo kutoka Leytonstone, Mashariki mwa London alisamehewa kufungwa gerezani kwasababu ana watoto wadogo wawili mmoja mwenye miaka minane na mwingine miezi 18.
Alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani na kuagizwa kufanya kazi kwa saa 90 bila malipo.
0 comments :
Post a Comment