RAIS AWAFUKUZA KAZI WAKUU WAWILI WA MAJESHI.

Rais wa Cameroon, Paul Biya, amewafuta kazi maafisa wakuu 2 wa jeshi baada ya wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram kutekeleza mashambulizi ndani ya nchi hiyo.
                                                      Na BBC SWAHIL.
Katika taarifa iliyopeperusha katika kituo cha redio ya taifa hakuna sababu yeyote iliyotolewa kwa kutimuliwa kazi kwa kanali Youssa Gedeon na luteini kanali Justin Ngonga.
Wadau wa maswala ya usalama katika magharibi mwa Afrika hata hivyo wanashauri kuwa huenda Biya ameanza kuhofia uwezo wa Boko Haram kutekeleza mashambulizi ndani ya Cameroon.

Rais Biya amewafuta kazi wanajeshi wawili kwa utepetevu

Jumapili iliyopita kundi la Boko Haram lilimteka mke wa naibu waziri mkuu .
Yamkini Boko Haram ilimteka pamoja na msaidizi wake kiongozi mmoja wa kidini pamoja na meya wa mji wa Kolofata.

Mwandishi wa BBC aliyeko Yaounde Cameroon Muhaman Babalala anasema tukio hilo la utekaji nyara lilidhibitisha utepetevu wa maafisa wa usalama nchini Cameroon.

Kundi la Boko Haram linaanza kupanua eneo la mashambulizi yake
Maafisa hao wawili walikuwa wakiongoza doria katika mpaka wa Cameroon na Nigeria.
Kundi la Boko Haram limekuwa likipigania kuundwa kwa taifa la kiislamu kaskazini mwa Nigeria lakini katika siku za hivi punde limetekeleza mashambulizi ndani ya ardhi ya Cameroon.
Wapiganaji hao wamelaumiwa kwa vifo vya wanajeshi wanne mbali na utekaji nyara wa wageni nchini Cameroon.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment