TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI.
Jose Mourinho hatomuuza Romelu Lukaku, 21, msimu huu (Sun), Arsenal wanajiandaa na maisha bila Thomas Vermaelen baada ya Manchester United kupanda dau la pauni milioni 10 kumchukua beki huyo wa Ubelgiji (Daily Star Sunday), AC Milan wanataka kumsajili Nani, lakini hawataki kutoa pauni milioni 11 wanazotaka Manchester United (Sunday Express), uhamisho wa Fabio Borini kutoka Liverpool kwenda Sunderland wa pauni milioni 14 bado uko kwenye ati ati kwa sababu mchezaji huyo wa Italia hataki uhamisho wa kudumu (Guardian), Barcelona wanamtazama beki wa kati wa Tottenham, Jan Vertonghen, 27 (Talksport), beki Ben Davies, 21, wa Swansea anajiandaa kwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na Tottenham mkataba ambao utamrejesha Gylfi Siggurdson kutoka Spurs kwenda Swansea (Guardian), Newcastle wanataka kumrejesha Andy Carroll kutoka West Ham, miaka mitatu na nusu baada ya kuondoka na kwenda Liverpool (Sunday People), Southampton wanamtaka Dusco Tosic, 29, kuziba nafasi iliyoachwa na Luke Shaw (Mail on Sunday), Arsenal wapo karibu kukamilisha mkataba wa pauni milioni 15.8 kumsajili Mario Balotelli, 23, kutoka AC Milan (Caught Offside).
Beki wa Uholanzi na Feyernoord Stefan de Vrij, 22, anajiandaa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Louis van Gaal tangu aanze kazi rasmi Manchester United kwa mkataba wa pauni milioni 10 (Sunday Mirror), Manuel Pellegrini yuko tayari kuonesha azma yake kusalia Manchester City licha ya Brazil kutaka kumpa kazi ya kuifundisha timu ya taifa kuchukua nafasi ya Luiz Filipe. Scolari (Sun), mipango ya Chelsea huenda ikaingia doa kufuatia taarifa kuwa kiungo Mohamed Salah, 22, huenda akatakiwa kurejea kwao Misri kutumikia jeshi (Sunday Expess), kiungo wa Newcastle Hatem Ben Arfa, 27, hajapewa namba atakayochezea katika msimu mpya (Daily Mirror), Louis van Gaal anafikiria kutotaja nahodha wake mpaka Michael Carrick atakapopona jeraha lake (Mail on Sunday), Van Gaal pia ametaka mabadiliko kufanywa kwenye uwanja wa mazoezi ikiwemo kuweka taa zaidi kuruhusu mazoezi ya usiku na vitanda kwa wachezaji katika mkakati wake wa mazoezi ya mara mbili kwa siku (Daily Star Sunday), Liverpool wamemuulizia Isco wa Real Madrid, ambaye pia anasakwa na AC Milan na Sevilla, ingawa mwenyewe anasema hataki kuondoka Bernabeu (AS), Sporting Lisbon wamekataa dau la pauni milioni 24 kutoka kwa Arsenal kumnunua William Carvahlo. Sporting wanataka takriban pauni milioni 35.6 (Metro), Juventus na Manchester United wamekubaliana mauzo ya Patrice Evra ambaye atasaini mkataba wa miaka miwili, na huenda ikathibitishwa siku ya Jumatatu (Gazzetta dello Sport), Manchester United wataanza tena kumfuatilia Edinson Cavani kutoka Paris St-Germain ikiwa Wayne Rooney atashindwa kumridhisha Louis van Gaal (Mail on Sunday). Hayo ndio yamejiri kwenye magazeti ya Jumapili, tetesi nyingine kesho tukijaaliwa- share hizi na wapenda soka wote. Cheers!!!!!
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment