Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo Neneka Rashid akitoa Taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo kwenye kikao Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Nsimbo.
(Picha Na Kibada Kibada –Nsimbo Katavi)
Na Kibada Kibada -Nsimbo Katavi
Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi kwa kipindi cha mwezi Februari mwaka huu ilifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 101,028,128 sawa na asilimia 22.23 ya lengo kwa mwezi.
Hayo yamelezwa na Makamo mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uongozi Slvester Nswima, wakati akiwasilisha Taarifa ya kamati hiyo kwenye kikao cha Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halamshauru hiyo.
Makamu Mwenyekiti huyo alieleza kuwa kwa kipindi cha mwezi mmoja (Februari), Halmashauri ilikusudia kukusanya jumla ya shilingi 451,507,275, lakini makusanyo halisi ilikuwa ni 101,028,128.50 sawa na asilimia 23.50
Aliendelea kueleza kuwa Mapato haya yanatokana na vyanzo vya mapato ambavyo ni ruzuku ya kawaida , vyanzo vya ndani,pamoja na mifuko mbalimbali ya maendeleo.
Awali akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo , Mohamed Assenga amesema kuwa pamoja na kufanikiwa kukusanya mapato pia zipo changamoto kadhaa zilizochangia kutofikia lengo ikiwa ni pamoja na mapokezi hafifu na kucheleweshwa kwa fedha za ruzuku ya maendeleo na matumizi ya kawaida toka Serikali kuu, hali iliyopelekea Halmashauri kupata wakati mugumu wa kutekeleza shughuli zake za kawaida.
Changamoto nyingine ni upungufu wa watumishi katika sekta mbalimbali za Halmashauri pamoja na Vijiji na Kata zilizopo .
Changamoto nyingine ni kukosekana baadhi ya vitendea kazi kama huduma za simu, Fax,magari na hata mitandao ya Internet kwa ajili ya kupokea na kutuma taarifa mbalimbali za Halmashauri.
Kukosekana na kupungua kwa nguvu kazi za wananchi za kutekeleza miradi ya maendeleo, hali inayosababisha kusimama kwa ujenzi na mara nyingine hata wakandarasi kutekeleza miradi .
Hata hivyo halmashauri imejipanga kukabiliana na changamoto hizo kuhakikisha inawaletea wananchi maendeleo kama ilivyojiwekea malengo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hamashauri hiyo, Neneka Rashid alieleza kuwa Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi milioni 350 katika bajeti yake kwa ajili ya miradi ya maendeleo .
Ambapo ameleza kuwa fedha hizo zitatumika kununulia vitendea kazi, magari matatu kwa ajili ya kusimamia shughuli za miradi katika Halmashauri,pamoja na shughuli za kiutawala, na ukaguzi wa miradi.
0 comments :
Post a Comment