MWANAMKE MWENYE ‘MAHIPS’ MAKUBWA AINGIA KATIKA KITABU CHA KUMBUKUMBU ZA GUINNESS

                        Mikel Ruffinelli ndiye mwanamke anayejulikana rasmi kuwa na ‘mahips’ makubwa zaidi duniani. Akiwa amepozi na mumewe, Reggie Brooks.
Kwa mujibu wa gazeti la ‘WorldWide Werid News’, Ruffinelli alikuwa na umbo la kawaida kabisa wakati wa ujana na hakuwa na tatizo lolote la kuongezeka uzito, lakini, akiwa na umri wa miaka 22, alianza kuona ‘mahips’ yake yanazidi kuongezeka baada ya kuzaa mtoto wake wa kwanza.

Aliongeza kusema kwamba kila alipokuwa anazaa, sehemu yake hiyo ya mwili ilizidi kuongezeka mpaka akawa anashindwa kupita kwenye mlango wa kawaida.  Japokuwa kiuno chake kina inchi 40 (sentimita 102), nyonga zake zinafikia inchi 100 (sentimita 254), hali inayomfanya avunje rekodi ya dunia.
 Pamoja na kwamba watu humshangaa kila anapopita na humwomba kupiga naye picha za kawaida na za video kutokana na umbo lake hilo, bado hujisikia mwenye furaha.

Anasema: “Ninapotembea mitaani, watu hunipiga picha za kawaida na za video kutoka kwenye simu zao.  Watu wengine hufikiri kwamba nilifanyiwa upasuaji ili kuupa mwonekano wa kupendeza mwili wangu, lakini ukweli ni kwamba umbo hili ni la asili.”

Ruffinelli hana mpango wa kupunguza unene wake, lakini anakiri kwamba umbo lake hilo humfanya  nyakati fulani akate tiketi  za viti viwili anaposafiri kwenye ndege, kwani kiti kimoja hakimtoshi.

Umbo lake humlazimu kupita kiubavu katika milango mbalimbali na huwa hawezi kufunga mlango wa bafu lake wakati akioga kwani sehemu ya mwili wake huwa imejitokeza nje.
                                         Mikel Ruffinelli akiwa katika pozi.
Mama huyo ambaye ni Mmarekani, anasema anajisikia raha mustarehe na umbo lake hilo alilo nalo.
Ruffinelli ambaye ni mama wa watoto wanne, mkazi wa Jimbo la California, Marekani, anasema anaishi maisha ya kawaida na kuendesha kazi zake vizuri ambapo mumewe, Reggie Brooks, pia humsifia kwamba anampenda jinsi alivyoumbika.
 Mikel Ruffinelli ndiye mwanamke anayejulikana rasmi kuwa na ‘mahips’ makubwa zaidi  duniani.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment