Mhubiri wa kiislamu Abu Hamza amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa makosa ya ugaidi katika mahakama moja mjini New York.
Alipatikana na hatia katika mashtaka kadhaa ikiwemo njama ya kuwateka nyara watu kutoka nchi za magharibi ikiwemo Yemen mwaka 1998 na majaribio ya kuanzisha kituo cha mafunzo ya ugaidi kwenye jimbo la Oregon nchini Marekani.
Jaji alisema kuwa Abu Hamza alikuwa amewachochea watu wengine kuwaua wale wasio waislamu kama jukumu la kidini na kusema kuwa alikuwa hatari kwa jamii.
Alifahamika kwa kutoa hotuba kali kwenye msikiti mmoja mjini London.
(CHANZO: BBC SWAHILI)
0 comments :
Post a Comment