MCHEZAJI WA DAR YOUNG AFRICAN HAMIS TAMBE AMVAA HANS POPPE.

Mshambuliaji wa Yanga, raia wa Burundi, Amissi Tambwe.
Na Mwandishi wetu
MSHAMBULIAJI wa Yanga, raia wa Burundi, Amissi Tambwe, amesikitishwa na kauli zilizotolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe  aliyekaririwa akizungumzia sakata la straika huyo kupigwa kabali na beki  wa Ruvu Shooting, George Michael katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyozikutanisha timu hizo wiki iliyopita.
Hans Poppe ambaye ana ushawishi mkubwa ndani ya Simba,  alikaririwa akisema kuwa, Tambwe pia alifanya makosa makubwa katika mechi hiyo, hivyo pia alistahili adhabu ya kadi nyekundu.
Kigogo huyo alienda mbali zaidi na kufikia hatua ya kusema kuwa, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linatakiwa kumpatia adhabu Tambwe kutokana na ubabe ambao na yeye aliuonyesha katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa.
“Hata sijui ni nini wanachonitafuta, nilipigiwa simu na watu wengi wakiniambia kuwa Hans Poppe kasema kuwa mimi nilimpiga ngumi Michael, hivyo nastahili kufungiwa.“Hakika hali hii imenisikitisha sana na sikutegemea kabisa kama Hans Poppe angesema maneno hayo ambayo hayapo, kila mchezaji aliyekuwa uwanjani siku hiyo anajua kila kitu ambacho Michael alinifanyia, kuna mambo mengine ni vigumu kuyazungumzia.
“Kusema kweli jambo hilo limenisikitisha sana na sijui ni kwa sababu gani Simba wamekuwa wakitendea mambo ya ajabu katika siku za hivi karibuni au kwa sababu  nipo Yanga? Namuachia Mungu,” alisema Tambwe.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment