Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amekubali kushindwa katika mpango wa mabadiliko ya umiliki wa ardhi nchini mwake.
''Ninafikiri Mashamba tuliyowapa Watu ni makubwa sana, hawawezi kumudu,'' alisema Kiongozi huyo mwenye miaka 91.
Mwanzoni alilenga kutupa lawama kwa kilimo duni, hali ya hewa na Vikwazo kutoka nchi za magharibi.
Kunyang'anya ardhi kutoka kwa Wakulima weupe, kumeonekana sababu kubwa ya kudorora kwa uchumi wa Zimbabwe tangu mwaka 2000.
Mwandishi wa BBC mjini Harare amesema si mara ya kwanza kwa Mugabe kukosoa Wakulima weusi.
Mugabe, alitaka kuwahamasisha Wakulima kujihusisha na kilimo cha Ngano,amewalaumu kwa uzalishaji duni wa Wakulima wanaolima mazao ya Biashara pia kwa kushindwa kutumia ardhi yote.
''Utawaona Wakulima wengi wanatumia theluthi moja tu ya Shamba zima,'' Gazeti la Serikali ya Zimbabwe, Herald lilimnukuu Mugabe.
Source BBC Swahil.
0 comments :
Post a Comment