KINANA: TAMASHA LA PASAKA LITUMIKE KUIOMBEA AMANI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ametoa wito kwa waandaaji wa Tamasha la Pasaka, Kampuni ya Msama Promotions kuongeza ufanisi kwa kuongeza chachu kwa waimbaji kuiombea amani Tanzania hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa Kinana sambamba na hilo kwa pamoja tuiombee nchi yetu umoja, amani, mshikamano ambako tamasha hilo litumike kumuomba Mungu kufanikisha umoja kwa Watanzania ulioasisiwa  na baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere.
Kinana alitumia fursa hiyo kuwatakia heri na fanaka Wakristo wote duniani heri na fanaka katika sherehe hizo ambazo ni kumbukumbu kubwa kwao ambayo haifanani na nyingine za kijamii.

Aidha Kinana alimpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama kwa kuwaunganisha Watanzania wa madhehebu mbalimbali na kuwa kitu kimoja na kudumisha mshikamano katika jamii. 

Kinana alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa mashabiki na wapenzi wa tamasha hilo kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha mipangilio ya Msama katika kuisaidia jamii ya Watanzania.

Kinana ni mmoja wa Makatibu wa CCM wanaotekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kuweza  kurudisha heshima ya chama kilichopoteza mwelekeo, hivi sasa CCM imerudisha heshima kama ilivyokuwa kwenye uongozi wa baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment