Wanajeshi wa Chadi nchini Nigeria.
Kundi la jihad lililoko Nigeria, Boko Haram, kwa mara ya kwanza limeshambulia Chad.
Wakuu nchini humo wanasema kuwa, wapiganaji wa Boko Haram walivuka ziwa Chad kwa maboti usiku na kushambulia kijiji cha Ngouboua, kilichoko kandokando ya ziwa hilo.
Liliwauwa watu, kuchoma moto vijiji vyao na kuiba mali.
Wapiganaji wa kundi la Boko haram wakilishambulia Taifa la Chadi
Chifu wa eneo hilo ni miongoni mwa waliouawa.
Majeshi ya Chad yanasemekana kuwarudisha nyuma wapiganaji hao ambao wanadhibiti eneo kubwa la ziwa hilo upande wa Nigeria.
Majeshi ya Chad yamekuwa yakikabiliana na Boko Haram nchini Nigeria taifa hilo ni la nne kushambuliwa na wapiganaji hao wa kiislamu.
Source BBC Swahil.
0 comments :
Post a Comment