Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi Akizindua Nakala ya Katiba Pendekezwa ili ziweze kugawiwa kwa Mkoa wa Katavi,kushoto kwa Mkuu wa Mkoa Ni Katibu Tawala wa Mkoa Mhandisi Emanuel Kalobelo pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa huo.
…………………………………………………………………
Na Kibada Ernest-Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahimu Hamisi Msengi amewaasa wakazi wa Mkoa huo kujenga utamaduni wa kusoma nyaraka mbalimbali ili kujijengea uelewa wa mambo muhimu, na amewasisitiza wananchi wa Mkoa huo kusoma nakala za Katiba inayopendekezwa ili siku itakapofika ya kwenda kuipingia kura wawe na umaamuzi sahihi.
Dkt Msengi ametoa Rai hiyo wakati wa kikao kati yake na Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, Wataalamu wa Kada mbalimbali, Taasisi za Serikali zilizopo katika Mkoa huo,Kamati za ulinzi na usalama Wilaya na Mkoa, Watendaji wa Mitaa,Wazee Mashuhuri na Viongozi wa Madhehebu ya dini kilichofanyika jana(juzi)kwenye ukumbi wa Mikutano Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Kikao hicho kilichoambatana na uzindua wa Nakala za Katiba pendekezwa zilizoletwa Mkoani Kataviili ziweze kugawiwa kwa wananchi waweze kuzisoma na kuzielewa kabla zoezi la kuipigia kura Katiba pendekezwa muda utakapofika.
Amesema watanzania wamekuwa na tabia ya kutopenda kusoma nyaraka muhimu hivyo kuwa na tabia ya kudharau mambo ambapo nyaraka hizo ni muhimu kama Katiba inayopendekezwa iwapo wataisoma wataweza kuelewa kwa undani kilichoandikwa na watakapokwenda kupiga kura watakuwa na uamuzi wa kufanya, kwa kuwa watakuwa wanafahamu kile kilichoandikwa ndani ya Katiba pendekezwa.pia unaweza kuisoma ukaelewa na ukashindwa kutoa maamuzi.
“Tuondokane na ugonjwa huu wa kutokusoma tuwe na tabia ya kujisomea ili tuwe na uhakika wa mambo tunayoyafanya”amesema Dkt Msengi.
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa rai kwa wakazi wote wa Mkoa huo kujenga tabia ya kusoma nyaraka, na waisome Nakala ya katiba iliyopendekezwa na kuielewa na muda ukifika wa kupiga kura wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura ili watumie haki yao ya kidemokrasia.
Akaongeza kuwa ili uwe na fursa ya kupiga kura lazima ujiandikishe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.ili uweze kupiga kura kwa mjibu wa sheria lazima ujiandikishe.
Wakati ukifika wa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura wananchi wajitokeze kwenda kujiandikisha na wale ambao hawataweza kujiandikisha watakosa fursa hiyo ya kidemokrasia ya kuipigia kura Katiba pendekezwa na kuwachagua viongozi wao ambao ni Madiwani Wabunge na Rais katika uchaguzi Mkuu utakapofanyika Oktoba mwaka huo.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Mhandisi Emanuel Kalobelo ameeleza kuwa Mkoa wa Katavi umepokea jumla ya Nakala 15,640,za Katiba Pendekezwa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili ziweze kugawiwa kulingana na maelekezo ya ugawaji wa nakala za katiba hizo.
Mhandisi Kalobelo ameeleza kuwa mgao wa Nakala hizo umegawanywa kwa mpangilio kama ilivyoelekezwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda iligawiwa nakala 3,900,Halmshauri ya Nsimbo Nakala 3,600,Halmashauri ya Mji Mpanda Nakala 3,600,Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Nakala 4,500, na wamekabidhiwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa.ambapo kwa upande wa Mkoa na taasisizilizopo katika mkoa huo ulipokea nakala 40 kwa ajili ya kuzigawa kwenye Taasisi zilizopo katika Mkoa huo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima akimkaribisha Mkuu wa Mkoa amewaeleza Viongozi wote kuwa wanatakiwa kufikisha ujumbe kwa wananchi wao na wawahamasishe wajitokeze kwa wingi katika zoezi la kujianadikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Pia amewasisistiza wapeleke nakala hizo kwa wananchi wazisome ili waweze kuwa na uamuzi wa kuipigia kura Katiba pendekezwa wakiwa na uelewa kuhusu Katiba hiyo Pendekezwa.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi ambaye pia ni Afisa Tawala wa Mkoa wa Katavi Salum Shilingi akawaasa Viongozi hao kuwa ni Nakala hizo haziuzwi zinagawiwa bure,na lengo lake ni kuwagawia bure wananchi wazisome ,atakayepatikana akiziuza hatua kali zitachukuliwa juu yake.
Katika Hatua nyingine akapongeza Gazeti la Mpandaleo kwa kueleimisha Jamii ya Mkoa wa Katavi na Mikoa jirani kutokana na habari zake zinazoandikwa humu akasisitiza wananchi waendelee kulisoma kwa kuwa ni kioo na kielelezo cha Mkoa.
0 comments :
Post a Comment