Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa(katikati) akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Shina la Pamba jijini Dar es Salaam, mapema jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kutambulisha jumuiya hiyo.Tawi hilo lipo katika Kata ya Kivukoni , Manispaa ya Ilala.Kulia ni Mwenyekiti UWT Kata ya Kivukoni Bibi. Rahilu Nyundo na kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Shina la Pamba Bibi. Sophia Mbwille.
Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa akipokea risala ya UWT Shina la Pamba kutoka kwa Mjumbe wa Jumuiya hiyo Bibi. Twihuvila Faith Nyimbo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano wa jumuiya hiyo.
Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa akifurahia jambo na wajumbe wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Shina la Pamba jijini Dar es Salaam, mapema jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kutambulisha jumuiya hiyo.Shina hilo lipo katika Kata ya Kivukoni , Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa UWT Shina la Pamba lililoko katika manispa ya Ilala jijini Dar es Salaam wakimskiliza mgeni rasmi ambaye ni Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija, MAELEZO.
0 comments :
Post a Comment