Na Anitha Jonas
MAELEZO
16/09/2014
Serikali imesema kuwa mradi wa gasi kutoka Mtwara hadi katika kituo cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu (2014) na kuanza majaribio Januari, 2015.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bwana Elihakim Maswi asema hadi sasa mradi huo wa gesi umekamilika kwa zaidi ya asilimia 70.
“Nimempa maelekezao mkandarasi wa mradi kila wiki aniletee taarifa nini alichokifanya wiki nzima ili nijue maendeleo ya mradi ulipofikia,” amesema.
Bwana Maswi ameeleza hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa mitambo ya gesi katika eneo la Kinyerezi. Ziara hiyo imeshirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini ikiwemo Benki ya Dunia, JICA, Umoja wa Mataifa (UN) na TPDC.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wizara ya nishati na Madini, kwa sasa hivi, uzalishaji wa umeme katika shirika la TANESCO unaigharimu serikali 1.6trilioni kwa mwaka.
Baada ya mradi huu kukamilika serikali itaokoa kiasi hicho cha fedha na kuzielekeza katika miradi mingine ya jamii.
Mradi wa gesi kutoka mtwara hadi Dar es Salaam utagharimu dola za Kimarekani 183 millioni, hadi sasa, serikali imekwishalipa Dola milioni 139 bado dola 44 millioni.
Kwa mujibu wa mwandisi wa mradi huo Simon Gilima, mradi huo unatarajia kuzalisha megawatt 150 zitakazoingizwa katika gridi ya taifa na kusaidia uzalishaji wa umeme kuwa wa uhakika na wa bei rahisi.
Amesema,“Mradi huu ukikamilika, utasaidia kupunguza gharama za uzalishaji wa umeme, na kuipunguzia serikali gharama za uzalishajii wa umeme.”
Mmoja wa wadau wa maendeleo nchini ambaye pia ni Mkurugenzi wa UN nchini Bwana Philippe Dongier ameelezea kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo na kusema utaongeza ajira nchini na kuongeza pato la taifa.
Amesma, “serikali iendelee kubuni miradi mingine kama huu itakayosaidia kuopunguza tatizo la ajira nchini.”
“Serikali iwe makini na masuala ya uwekezaji kwa kulinda na kusimamia sera za nchi ikiwemo matakwa ya nchi.” Alisema Bwana Philipe.
0 comments :
Post a Comment