Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria ishara ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya CCM wilaya ya Mafia.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akifanya mzaha na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye mara baada kukagua mradi wa maji,masaidia zaidi ya mradi huu wa maji utahudumia watu zaidi ya 3000.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya mashua kutoka kwa Katibu wa CCM wilaya wa pwani
Sehemu ya vifaa vya mkandarasi vikiwa kwenye eneo linapotengenezwa tuta la Banjo,ujenzi wa tuta hili utasaidia sana wakazi wa vijiji vya Banja na Jojo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimwonyesha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman taarifa mbali mbali kutoka kwenye blogs, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na upande wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwinshehe Mlao.
Katibu Mkuu wa CCM, akipanda boti ya kizamani, tayari kwa ajili ya safari kutoka Kisiwa cha Mafia kwenda Nyamisati wilayani Rufiji, baada ya kumaliza ziara yake katika wilaya ya Kisiwa hicho, leo Septemba 17, 2014, akiwa katika ziara ya mkoa wa Pwani, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoahuo. Boti hiyo ambayo pia hutumiwa na wananchi kusafiria kati ya kisiwa hicho cha Mafia na Nyamisati Kinana amesafiri nayo kwa saa nne tangu saa sita mchana hadi saa 11 jioni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Mafia.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment