KINANA HII NI SIASA AU NI UHALISIA WA KAZI?

Katibu  Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishona nguo kwenye ofisi ya Veronica Simba (kushoto) iliyopo Mombo Sokoni,kulia ni Mbunge wa Korogwe Vijijini Ndugu Stephen Ngonyani ,Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya siku moja katika wilaya ya Korogwe Vijijini ambapo licha ya kukagua miradi mbali mbali ya ujenzi wa maabara na ofisi za CCM alipata nafasi ya kuwahutubia wananchi na kuwasikiliza  .
Katibu  Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuelekeza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kushona nguo kwenye ofisi ya Veronica Simba (kushoto) iliyopo Mombo Sokoni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Ueneziwakinunua matunda kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara Mombo.
Diwani wa kata ya Mombo akishangiia baada ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kutamka wazi kuwa katika kuhakikisha wanapata halmashauri ya mji mdogo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akiwapungia watu wakati wa kuwasili kwenye uwanja wa mikutano mjini Mombo akiwa pamoja  na Katibu wa NEC Itikadi Nape Nnauye.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mombo ambapo aliwaambia wananchi hao wanachofanya wapinzani ni biashara, kwani kwao kuandamanisha watu ni mtaji mzuri wa kuwaingizia pesa kutoka nje.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mombo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa kwenye kiti tayari kupokea zawadi kutoka kwa wamasai wanaoishi Mombo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi kutoka kwa wamasai wa Mombo.
 Katibu wa CCM Ndugu Abdulrahman akipeana mkono wa shukrani kwa kiongozi wa wamasai wa Mbombo Samng'o Maikaambaye [ia ni mwenyekiti wa Tawi la Chang'ombe ,Mombo.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment