MASHINDANO YA SKAUTI NGAZI YA TAIFA YAFUNGWA RASMI MKOANI MOROGORO SEPTEMBA 26,2014

Kamishina Mkuu Msaidizi Programu ya Vijana wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA), Mary Anyitike (kushoto), akimvisha  Nishani ya Skauta, Safi Shabani kiongozi wa Skauti kutoka  Shule ya Sekondari Lugoba iliyopo Bagamoyo mkoa wa Pwani wakati wa hafla ya kufunga mashindano hayo jana.
 Kamishina Mkuu Msaidizi wa Utawara Bora wa wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA), Mwalimu mstaafu John Lusunike (kushoto), akikagua skauti kabla ya kuanza mashindano Septemba 23,2014. 


………………………………………………………
Dotto Mwaibale

MASHINDANO ya Skauti ngazi ya Taifa ya  Chama cha Skauti Tanzania (TSA), yaliyoanza Septemba 14, 2014 na kushirikisha vijana wa skauti kutoka mikoa minne ya Tanzania Bara yamefungwa rasmi mkoani Morogoro jana.
Akizungumza na mtandao wa www.habari za amii.comKamishina Mkuu Msaidizi Programu ya Vijana wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA), Mary Anyitike alisema mashindano hayo yamekwenda vizuri na kuongeza weredi wa masuala mbalimbali kwa vijana hao.
“Mashindano ya namna hii hufanyika kila mwaka na kushirikisha vijana kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara ili kupata skauti watakao wakilisha nchi kwenye mashindano ya skauti ya Afrika Mashariki yanayofanyika kila mwaka” alisema Anyitike.
Alisema changamoto kubwa iliyopo ni ushiriki mdogo wa vijana wa skauti kutoka mikoani unaosababishwa na uzembe wa baadhi ya makamishina wa mikoa kwa kushindwa kutilia mkazo wa kushiriki mashindano hayo muhimu.


Anyitike alisema changamoto nyingine ni suala zima la kiuchumi kwani shughuli nyingi za skauti ni za kujitolea hivyo skauti wengi hukosa nafasi kujumuika na wenzao katika jambo hilo.
Alisema kuwa mwaka huu ni mikoa minne tu kati ya mikoa yote ya Tanzania Bara iliyoshiriki mashindano hayo ambayo ni mkoa wa Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Shinyanga.

Alisema katika mashindano hayo skauti hao walijifunza mambo mengi pamoja na mafunzo ya kilimo hai yaliyotolewa na Taasisi ya Sustainable Agriculture Tanzania (SAT) ambayo inafanya shughuli zake mkoani Morogoro.


Alisema mafunzo hayo ni muhimu sana katika suala zima la kilimo kwanza hasa wakati huu wa matokeo makubwa sasa (BRN) na suala zima la kukabiliana na ajira hapa nchini kwa kundi la vijana ambao wengi wao wanakimbilia mijini kutafuta kazi za kuajiriwa ambazo hazipo.


Mashindano ya Skauti ya Afrika Mashariki yanayo husisha nchi za Uganda, Kenya, Ruanda, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini na Tanzania yanatarajia kufanyika nchini Rwanda Desemba mwaka huu ambapo washindi wa mashindano hayo yaliyofungwa jana watawakilisha taifa kwenye mashindano hayo.
      Vijana wa skauti wakiwa katika maandalizi ya kupangiwa kazi.
   Vijana wa Skauti wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa tayari kwa ukaguzi.
Vijana wa Skauti wa Kikosi cha Simba kutoka Mkoa wa Morogoro ambao walikuwa washindi wa Mashindano ya Skauti katika nchi za Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Burundi mwaka 2013 wakiwa tayari kwa ukaguzi huo kabla ya mashindano hayo yenye lengo la kuwapata washiriki katika mashindano ya Afrika Mashariki yatakayofanyika nchini Rwanda Desemba 2014.
 Vijana wa Skauti wakijifunza Kilimo Hai jinsi ya kuandaa shamba mfuko bila kutumia mbolea zisiso na kemikali.
                                      Hapa vijana wa skauti wakipika chai wakiwa juu ya mti.
               Vijana wa skauti wakijadili maswali ya kazi walizopewa.
           Hapa wakiwa wamepumzika kwenye vitanda vya miti.
                Vijana hao wakisubiri kupatiwa maelekezo na viongozi wao.
 Kamishina wa Skauti Mkoa wa Morogoro, Francis Gasper Francis kwa niaba ya Kamisha Mkuu wa TSA, akimuapisha Kamishina wa Wilaya ya Kilosa ndugu Miraji.

 Kamishina Mkuu Msaidizi Programu ya Vijana wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA), Mary Anyitike (kushoto), akimpa maelekezo, Safi Shabani kiongozi wa Skauti kutoka  Shule ya Sekondari Lugoba iliyopo Bagamoyo mkoa wa Pwani wakati wa hafla ya kufunga mashindano hayo jana.
Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062


About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment