afisa mawasiliamo ya TGNP Bw Melikizedeck Karol wakati akitoa mada ya uchaguzi mkuu
Na matukiodaimaBlog, Mbeya
WAKATI vuguvugu la uchaguzi mkuu mwaka 2015 likiendelea kushika kasi ndani ya vyama vya siasa kwa wanachama mbali mbali kujitokeza kutangaza nia ,mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) umewataka wanawake nchini kujitokeza kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais .
Wito huo umetolewa afisa mawasiliamo ya TGNP Bw Melikizedeck Karol wakati akitoa mada ya ushiriki wa wanawake kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015 wakati wa mafunzo ya siku mbili ya wanahabari mikoa ya nyanda za juu kusini yaliyomalizika leo jijini Mbeya.
Alisema kuwa usawa katika nafasi za uongozi wa kutaka kuwa na asilimia 50 kwa 50 kati ya wanawake na wanaume ni lazima utimie katika uchaguzi huu kwa wanawake kuanza kujitokeza kuwania nafasi mbali mbali zikiwemo za juu kama Urais ,ubunge na udiwani .
Karol alisema kuwa kasi ya wanawake na vijana kujitokeza katika nafasi mbali mbali za uongozi inapaswa kuanza kujionyesha kuanzia sasa ili ikiwezekana bunge la baada ya uchaguzi mkuu 2015 idadi ya vijana na wanawake iongezeke zaidi bungeni.
"Hivi wataka kusema hakuna mwanamke katika nchi hii ambae anaweza kuongeza nchini kama Rais na kama wapo kwanini hawajitokezi kugombea nafasi za juu kama Urais .....lazima wanawake wachangamkie nafasi hiyo "
Kwani alisema kuwa katika jamii mwanamke ndie anayekumbwa na changamoto mbali mbali katika jamii na kuwa iwapo wanawake wataendelea kuwa nyuma katika kuwania nafasi hizo bado changamoto zilizopo zitaendelea kuwatesa wanawake .
Alisema kwa mwaka 2005 kuwa akidi nzima ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ni wabunge 357 kwa mujibu wa katiba hata hivyo viti maalum pekee ni 102 sawa na asilimia 28.6 vilivyogawanywa miongoni mwa vyama vya siasa kwa kuzingatia matokeo ya uchaguzi kati ya viti 239 vya majimbo (vikiwemo kutoka Zanzibar) ni wanawake 21 tu sawa na asilimia 8.8 ndio walipewa viti vya kuchaguliwa bungeni.
Huku idadi ya madiwani wa kuchaguliwa asilimia 4 na wenyeviti wa vijiji ni asilimia 2 wakati wenyeviti wa vitongoji ni asilimia 3 .
Hivyo alisema ni wajibu kwa vyombo vya habari na wanawabari nchini kuendelea kuhamasisha makundi ya vijana na wanawake kujitokeza kwa wingi katika nafasi za udiwani ,ubunge na Urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Alisema kuwa sera ya Taifa ya vijana pamoja na mkataba wa vijana wa Afrika unalitambua kundi la vijana kama ni rasilimili mojawapo muhimu sana kwenye maendeleo na pia katika kulinda amani na utulivu kwenye bara la afrika.
"Hata hivyo pamoja na kwamba vijana ni zaidi ya asilimia 60 bado mchango na thamani ya vijana haujulikani ipasavyo kwenye Demokrasia ya Tanzania huku thamani yao ikionekana tu nyaraka za uchaguzi kwa kutumiwa kama walinzi au wapambe wa wagombea"
Alisema ni vema vijana kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kutumia haki yao ya msingi ya kuchaguliwa na kuchagua .
|
0 comments :
Post a Comment