MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AZINDUA MPANGO WA KUWAINUA VIJANA WENYE VIPAJI VYA SANAA UJULIKANAO KINONDONI TALENT SEARCH

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akizindua mpango wa kuwainua vijana wenye vipaji vya sanaa mbalimbali ujulikanao kama Kinondoni Talent Search. Kulia ni Mwanamuziki, Peter Msechu na Emanuel Mathias ambaye ni mchekeshaji maarufu 'MC Pilipili ambao watasaidia kuratibu jinsi ya kuwatambua vijana hao katika wilaya hiyo.
DC Makonda akiwa amekaa na wanakamati watakaoshughulikia  mpango huo. Kutoka kulia ni mwanamuziki Peter Msechu, Mchekeshaji maarufu, Emanuel Mathias 'MC Pili pili', Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera na Ofisa Utamaduni wa Wilaya hiyo, Jumanne Mrimi.
 Mwanamuziki,  Peter Msechu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni DC Makonda.
 Mchekeshaji maarufu, Emanuel Mathias 'MC Pilipili' akizungumza kwenye mkutano huo.
Wanamuziki wakichukua taarifa hiyo.

Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ameandaa mashindano maalum ya wenye vipaji kupata nafasi ya kutoka kisanii liiitwalo kama
 'Kinondoni Talent Search'.

Akizugumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo asubuhi, Makonda alisema lengo kubwa la kuinua vipaji kwa vijana na kuwapatia fursa za kimaendeleo kupitia fani zao.
 
Makonda alisema kuwa 'Kinondoni Talent Search' ni mpango wenye lengo kuu la  kuwatambua vijana waishio kwenye wilaya ya Kinondoni wenye vipaji vya kuimba, kucheza na kuchekesha ambao wengi wao wapo katika mazingira magumu kiuchumi.

Alisema mchakato huo unalenga kuwatengenezea nafasi za mafanikio vijana wenye vipaji, kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na wadau muhimu waliopo katika sekta zao, lakini kubwa zaidi ikiwa ni kutoa hamasa kwa vijana wote wa kinondoni.

Makonda alisema mashindano hayo yatawafanya vijana kuepukana na mambo yanayoweza kuharibu malengo yao ya baadae mfano mzuri  ni matumizi ya dawa za kulevya,ngono zembe na vitendo vya uporaji.

"Ukimiliki kipaji unakuwa unamiliki ajira,ni  kujua tu namna ya kukitumia ili kikufae na kukufikisha  utakapo na ndio maana kauli mbiu
ya mpango huu ni kipaji chako ajira yako," alisema Makonda.

Mashindano hayo yatakayosimamiwa na Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni yamezinduliwa rasmi jana, Mkuu huyo waWilaya akitangaza kamati maalumu itakayosimamia zoezi hilo, yenye wajumbe watano kutoka ofisi yake pamoja na baadhi ya wasanii.

Aliwataja wajumbe wa kamati hiyo kuwa ni Jumanne Mrimi ambaye ni Ofisa Utamaduni wa wilaya hiyo, Sebastian Mhowera  Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni huku  ikiwahusisha wasanii wa muziki Peter Msechu ,mwanamitindo, Jokate Mwengelo na mchekeshaji maarufu Mc-pilipili.

Makonda alisema Kinondoni Talent Search itachukua takribani mwezi mmoja na nusu, huku ukijumuisha shughuli za utafutaji vipaji ambapo utaanzia ngazi ya kata 34 ambapo kutakuwa na mafunzo kwa washiriki, kuwapa nafasi washiriki kukutana na wadau mbalimbali wanaofanya kazi kama zao.

Aliongeza kuwa mwisho wa kufunga zoezi hilo kutafanyika tukio kubwa lenye hadhi ya kimataifa  litakalowapa vijana wote nafasi ya kuonesha vipaji vyao mbele ya mabalozi toka nchi mbalimbali kama sehemu ya mkakati wa kuwasogeza na wasanii kimataifa.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment