Mwanaharakati Alexei Navalny
Mwanaharakati maarufu anayepinga ufisadi nchini Urusi Alexei Navalny ameachiliwa baada ya kuzuiliwa kwa siku 15 gerezani.
Alikamatwa kwa kusambaza vijikaratasi mjini Moscow ikiwa ni kesi ya hivi punde kati ya kesi kadha zinazomkabili.
Mwezi Disemba bwaba Navalny na nduguye walipatikana na hatia ya ufisadi kwenye kesi ambayo wanasema ilichochewa kisiasa ambapo walihukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitatu.
Hatahivyo mwanaharakati huyo hakuruhusiwa kuhudhuria mazishi ya kiongozi wa upinzani Boris Nemtsov ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi wiki moja iliyopita.
0 comments :
Post a Comment