Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini taarifa iliyokuwa inasomwa na Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Paul Masanja (hayupo pichani)
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Singida (Viti Maalum) Martha Malata akisisitiza jambo katika kikao hicho.
…………………………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Arusha
Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Paul Masanja amesema kuwa Serikali imejipanga kuimarisha ulinzi ndani ya machimbo ya tanzanite ya Mirerani yaliyopo katika wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara
Mhandisi Masanja aliyasema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwenye kikao chake na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini wanaosimamia sekta za madini kilichofanyika jijini Arusha jana. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ipo mkoani Arusha kwa ajili ya kutembelea miradi mbalimbali ya umeme pamoja na kuzungumza na watendaji.
Mhandisi Masanja aliyasema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwenye kikao chake na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini wanaosimamia sekta za madini kilichofanyika jijini Arusha jana. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ipo mkoani Arusha kwa ajili ya kutembelea miradi mbalimbali ya umeme pamoja na kuzungumza na watendaji.
Aidha kamati hiyo, ilikutana na watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) na Wakala wa Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa ajili ya kupokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi na kutoa maazimio na mapendekezo mbalimbambali.
Mhandisi Masanja alisema kuwa Serikali ilijenga uzio wenye urefu wa kilomita 10 kwa gharama ya shilingi milioni 300 na kuongeza kuwa bado serikali ina mpango wa kujenga vibanda kwa ajili ya walinzi ili kupunguza wachimbaji haramu kuingia ndani ya maeneo ya uchimbaji wa madini hayo na kutoroka na tanzanite.
Alisema pamoja na kuimarisha ulinzi kwenye maeneo ya mgodi, Serikali imepanga kujenga kituo kikubwa kwa ajili ya biashara ya madini aina ya vito kitakachojulikana kwa jina la “Madini House” ambapo kutafanyika biashara ya madini hali itakayopunguza utoroshwaji wa madini yanayopelekwa nje ya nchi.
Aliongeza kuwa uanzishwaji wa kamati ya usalama kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya, kituo cha polisi umechangia kuimarishwa kwa ulinzi katika eneo la mgodi na kusisitiza kuwa bado serikali inabuni njia nyinyine zaidi za kisasa kwa ajili ya kudhibiti utoroshwaji wa madini ya tanzanite nje ya nchi.
Akielezea changamoto katika eneo ya Mirerani Mhandisi Masanja alisema kumekuwepo na migogoro ya wachimbaji wenyewe kwa wenyewe kugombea ardhi na kutokuzingatia sheria na kanuni za uchimbaji madini hali inayopelekea ajali za mara kwa mara mgodini.
“ Kule kwenye eneo la mgodi kuna uchimbaji hatari unaofanyika chini kwa chini ambapo wamejiwekea utaratibu wa kuwa, mchimbaji anapokutana na mwenzake kwenye mkondo wa madini chini ya ardhi, anatakiwa kurudi nyuma hatua kumi lakini bado kumekuwepo na changamoto ya wachimbaji kuvamia maeneo wanayohisi madini yapo bila kuzingatia kanuni za uchimbaji madini,” alisisitiza Mhandisi Masanja.
Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni pamoja na maeneo ya uchimbaji kuwa madogo na kuongeza kuwa ili kukabiliana na changamoto ya migogoro aliwashauri wachimbaji wadogo kuunda umoja kwa kuunganisha maeneo yao na kuomba leseni ya pamoja hali itakayowaongezea kipato huku ikipunguza migogoro isiyo ya lazima.
“ Kwa mfano iwapo wachimbaji wataungana ya kuomba leseni ya pamoja na kuchimba madini, kila mchimbaji ana uhakika wa kupata faida ya shilingi milioni 500 kwa mwaka,” alisema Mahandisi Masanja
Wakichangia kwa nyakati tofauti wajumbe kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini waliitaka Serikali kuongeza juhudi zaidi katika usimamizi wa sekta ya madini ikiwa ni pamoja na suala la ulinzi kwenye migodi hususan katika eneo la Mirerani.
Wakichangia kwa nyakati tofauti wajumbe kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini waliitaka Serikali kuongeza juhudi zaidi katika usimamizi wa sekta ya madini ikiwa ni pamoja na suala la ulinzi kwenye migodi hususan katika eneo la Mirerani.
Akichangia hoja katika kikao hicho mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Singida (Viti Maalum) Martha Mlata alisema kuwa mbali na kuimarisha ulinzi katika eneo la Mirerani kwa kuweka uzio na vibanda kwa ajili ya walinzi, vitambulisho kwa ajili ya wachimbaji wa mgodini vinatakiwa kutengenezwa vikiwa na majina ya makampuni yanayochimba madini.
Alisema kufanya hivyo, kutapunguza wimbi la wachimbaji haramu na wahamiaji wanaoingia katika maeneo hayo na kutoroka na madini hayo.
Mlata alisisitiza kuwa makampuni yanayoshindwa kulipa kodi kwa kisingizio cha kupata hasara yasivumiliwe kamwe , ikiwezekana yanyang’anywe leseni za madini.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Richard Ndassa alisema kuwa muarobaini wa utoroshwaji wa madini ya tanzanite unaweza kupatikana kwa kujenga ukuta mkubwa imara na kuitaka Serikali kuwa na mikakati zaidi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika eneo la Mirerani.
Ndassa alisema kuwa suala la usimamizi wa sekta ya madini halihitaji siasa, na kuwataka wajumbe wa kamati hiyo kuwa wazalendo badala ya kuweka siasa zaidi kwenye usimamizi wa sekta ya madini.
“Madini ya tanzanite yanapatikana Tanzania pekee duniani, hivyo ni vyema kuhakikisha madini haya yanalindwa kwa nguvu zote pamoja na usimamizi wake bila kuongozwa na siasa,” alisema Ndassa
“Madini ya tanzanite yanapatikana Tanzania pekee duniani, hivyo ni vyema kuhakikisha madini haya yanalindwa kwa nguvu zote pamoja na usimamizi wake bila kuongozwa na siasa,” alisema Ndassa
0 comments :
Post a Comment