WAMILIKI WA INTERNET WAASWA KUTOWARUHUSU WATOTO KUANGALIA PICHA ZA NGONO.

Na Mwandishi wetu.
Wamiliki wa Internet Cafe jijini hapa wametakiwa kuwa makini na wateja wao hususani watoto wadogo ambao hutumia huduma hizo kinyume kwa kuangalia Picha za ngono ambapo huchangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa maadili ya mtoto wa Kitanzania.

Wito huo umetolewa leo jijini hapa na Kamanda wa polisi wa jiji hili la  Arusha liberatus Sabas alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema amekuwa akisikitishwa na watoto wa karne hii ya sasa kwa kupenda kuangalia Picha hizo ambazo Haziwezi kuwajenga Kimaadili.

Alisema hivi sasa watoto wengi wamekuwa wakijidanganya asa kwa kupenda kufanya vitu ambavyo havina manufaa kwa maisha yao ya Baadae kitendo kitakachowafanya wje kuwa na muelekeo mbaya katika maisha yao ya baadae.

“Sidhani kama watoto wetu watakuja kuwa na masiha mazuri hapao baadae kwani abadala ya kujitahidi kuongeza bidii katika masopmo ambapo ndio mkombozi wa maisha yao Jamii kwa ujumla tuwakomboeni watoto wetu”Alisema kwa masikitiko makubwa.

Pia aliwaomba wazazi kuwa makini na watoto wao huku wakijitaidi wanakuwa katika hali inayostaili kimaadili ya mtoto wa kitanzani badala ya kuwaacha waige utamaduni wa kizungu ambapo hautakuwa na faida yeyote katika maisha yao ya Baadae.

“wapo baadhi ya wazazi hhupenda watotot wao kuiga tamaduni za kizungiu kuanzia mavazi wanayovaa wataoto hao mpaka katika saula zima la kimaadili,Sisis ni Watanzania jamani achaeni mitindo ya kuiga tunawafundisha nini watoto wetu jamani?”alihoji kwa jazba Matei.

Akiendelea kuzungumzia suala hilo kamanda Matei alisema endapo wazazi kwa kushirikiana na jamii kwa ujumla kukubali watoto wao kukanywa na kila pindi wanapokutwa waiaangalia picha hizo basi kwa namna moja ama nyingine wataweza kupunguza tatizo ingawa si wazazi wote wanaopenda watoto wao kurekebishwa na watu wengine pindi wanapokosea.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment