OLOLOSOKWAN WAJIWEKA TAYARI KUTIMIZA NDOTO YA KIJIJI CHA DIJITALI

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliposimama kwenye Kijiji cha Ngeresero kwa ajili ya kuwaungisha wanawake wa kimasai wanaofanya biashara ya kuuza bidhaa mbalimbali za shanga kwa watalii wanaosimama kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kupata mahitaji mbalimbali, wakati akielekea kijiji cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika lake la UNESCO.

Na Mwandishi wetu, Arusha
NDOTO ya kuwa na kijiji cha dijitali nchini Tanzania itaanza kutimia Januari mwakani wakati vifaa vinavyotakiwa kukamilisha mradi huo vitakapowasili kutoka kampuni ya Samsung Electronics.

Kwa mujibu wa watekelezaji wa mradi huo mkubwa unaotarajiwa kutumia dola za Marekani milioni 1, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) vifaa hivyo vinatarajiwa kuingia Bandari ya Dar es Salaam Januari tano mwakani.

Mkataba wa kuanzishwa kwa kijiji cha dijitali eneo la Ololosokwan tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro ulitiwa saini kati ya Unesco na Samsung electronics Novemba 6 mwaka huu.

Akizungumza na halmashauri ya kijiji cha Ololosokwan , Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues amewataka wanakijiji kujiandaa kwa mabadiliko makubwa ya kijiji chao kinapoingia katika dunia ya dijitali.
Alisema mambo ambayo wanastahili kuyaweka sawa ili kufanikisha ndoto zao kuhakikisha eneo ambalo mitambo na miundombinu ya mradi ipo ni lazima lisajiliwe kisheria ili kusiwepo na tatizo katika siku za usoni.

Aidha kutokana na ukubwa wa mashine zinazohusika, hasa makontena ni vyema wanakijiji wakaangalia maeneo korofi katika barabara za kuelekea huko na kuzirekebisha, ili magari hayo makubwa yenye vifaa yapite kwa usalama.

Alisema mradi huo wa miaka mitatu unatarajia kuwawezesha wananchi wa eneo hilo kuwa na ujasirimali, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika mawasiliano na utafutaji wa masoko, elimu na afya.

Kwa mujibu wa Bi. Rodrigues kijiji hicho pia kitakuwa na shule iliyoungwa na mtandao wa kompyuta duniani (intaneti), kliniki ya kisasa, tiba kwa kutumia teknolojia ya kompyuta na jenereta kubwa linalotumia nishati ya jua.
Bw. Abdulaziz Ali wa kitengo cha Transportation and Logistic kutoka UNESCO akitafsiri bei za bidhaa hizo za kimasai kwa wakimama hao wanaofanya biashara za urembo wa shanga kwa watalii na wazawa wanaopita katika kituo kijiji hicho ambapo wengine wao husimama kupata huduma ya chakula na vinywaji.

Aidha kuwapo na mtandao wa kompyuta kutawezesha UNESCO kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuanzisha mtaala utakaowawezesha vijana wa kimasai ambao ni wafugaji kupata elimu wanayoihitaji.

Mwakilishi huyo wa UNESCO amesema kwamba amefurahishwa na namna watu walivyoitikia mradi huo ambao umelenga kubadili maisha ya wafugaji hao kwa kuwawezesha pia kuitumia vilivyo sekta ya utalii.

“Kupitia mradi huu wananchi wanaweza kujifunza kusoma, kupata maarifa na katika harakati hizo kujua lugha ya kiingereza ili kuwasaidia kuwa na mawasiliano na watalii na watu wengine”, alisema Rodrigues.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwasili kwenye kata ya Ololosokwan kijiji cha Ololosokwan na kupokelewa na diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ndoinyo.

Alisema ni nia ya Unesco kuhakikisha kwamba inasaidia kufuta ujinga miongoni mwa wafugaji hao bila kuathiri utamaduni wao wanapoingia katika maisha ya kisasa.

Kijiji cha digitali cha Ololosokwan kitakuwa cha nne barani Afrika na yapo makubaliano ya msingi kwamba kijiji kingine kitajengwa Zanzibar mwakani.
Diwani wa kata ya Ololosokwan, Bw. Yannick Ndoinyo akiongozana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyefika kijijini hapo kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la UNESCO pamoja na kukagua eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kijiji cha digitali cha Samsung.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisalimiana na baadhi ya kinamama wa mradi wa utalii unaofadhiliwa na shirika la UNESCO kata ya Ololosokwan kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza na wakina mama wa kimasai waliojumuika na waume zao mara baada ya kuwasili kijijini hapo ambapo aliwaasa kushiriki elimu ya afya ya uzazi wa mpango ili waweze kuzaa watoto wachache watakaoweza kuwahudumia na aliwaahidi kuwaanzisha program ya kusoma na kuandika kwa ajili ya kuboresha mawasiliano yao na watalii wanaotembelea kijiji chao na kununua biashara zao.
Pichani juu na chini ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwaonyesha jambo wakina mama wa kimasai jinsi gani teknolojia inayvowaleta watu kwa ukaribu zaidi kupitia "Tablet" ambapo katika kijiji hicho cha digitali cha Samsung wakazi wa eneo hilo watakua wakipewa mafunzo kutumia kifaa hicho cha "Tablet".
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifafanua jambo nje ya maktaba inayofadhiliwa na UNESCO na kuwanufaisha wanafunzi wa shule ya sekondari Ololosokwani na vijana wa kata hiyo kupanua uelewa zaidi kwa kusoma vitabu mbalimbali wakati akikagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika lake. Kushoto ni Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ndoinyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwa kwenye mazungumzo na viongozi wa juu wa halmashauri ya kijiji wakati wa ziara yake kijijini hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja na uongozi wa halmashauri ya kijiji cha Ololosokwan mara baada ya mazungumzo.
Bi. Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja na baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Ololosokwan kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja na wakina mama wa kimasai wa kata ya Ololosokwan kijiji cha Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani Arusha mara baada ya kikao na halmashauri ya kijiji hicho.
Bi. Zulmira Rodrigues akiagana na baadhi ya wakinamama wa kimasai mara baada ya kikao cha halmashauri ya kijiji hicho.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) akifafanua jambo wakati wa kukagua eneo ambalo mitambo na miundombinu ya mradi itawekwa kwenye sehemu iliyotengwa na halmashauri ya kijiji kwa ajili ya kijiji cha dijitali cha Samsung. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya RAMAT, Pokare Koitumet, Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ndoinyo pamoja na Chifu wa kijiji cha Ololosokwan kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha.
Muonekano wa eneo hilo huku Bi. Zulmira Rodrigues akiendelea kulikagua.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment