TEWUTA YATOA MWITO KAMPUNI YA BHART AIRTEL KUJIONDOA UBIA KATIKA KAMPUNI YA SIMU YA TANZANIA (TTCL).

  Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (Tewuta), Junus Ndaro.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (Tewuta), Junus Ndaro (wa tatu kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,wakati akitoa  wito wa kujiondoa ubia kwa Kampuni ya Bhart Airtel katika Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Kutoka kulia ni Mfanyakazi wa Tewuta, Rashid Rajab, Mwanasheria Beatrice Monyo, Mwenyekiti Taifa wa Tewuta, Pius Makuke, Mwanasheria, Leila Farijalah na Ofisa wa Masijala, Ericla Frank.
 Mwenyekiti Taifa wa Tewuta, Pius Makuke (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Dotto Mwaibale

Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wameitaka Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Bhart Airtel kujitoa ubia ndani ya TTCL.

Mwito huo umetolewa na  Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (Tewuta), Junus Ndaro kwa niaba ya wenzake wakati akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi.

Alisema ni mara nyingi wamekuwa wakiitaka kampuni hiyo kuondoka ndani ya TTCL bila  mafanikio jambo ambalo ni kuifanya TTCL ishindwe kujiendesha.

Alisema tangu Bhart Airtel ipewe mkataba wa ubia ndani ya TTCL wa umiliki wa wa hisa asilimia 35 imeshindwa kuwekeza na kuiboresha kampuni hiyo kama walivyokubaliana hivyo kusababisha TTCL kujiendesha kwa hasara.

"Kitendo cha Bhart Airtel kuendelea kumiliki hisa zake hizo katika Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL) ni sawa na kitendo cha kuihujumu TTCL, na  kuwa toka mwaka 2012 Celtel walitoa taarifa ya awali ya kujiondoa ndani ya TTCL, na kuanzisha majadiliano ya uvunjaji wa mkataba baina ya pande zote mbili" alisema Ndaro

Ndaro aliongeza kuwa hadi sasa majadiliano hayo yamekuwa yakicheleweshwa na mwenye hisa ndogo pasipo kuwepo kwa sababu za msingi, kitendo hiki ni sawa na hujuma, mmiliki mdogo mwenye hisa anatambua kuwa TTCL haiwezi kupata mtaji mahali popote pasipo idhini yake.

Alisema Tewuta inapongeza juhudi zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine wa serikali kwa kuwaunga mkono kufuatilia jambo hilo na kuhakikisha wabia hao wanaondolewa ndani ya TTCL.

Ndaro ametumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kuungana katika jitihada za kuwaondoa wabia hao Bhart Airtel ambao wanaihujuma Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). (Imeandaliwa na mtandao

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment