Katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi, wenyeji Azam FC walimaliza mwendo mbaya wa vipigo baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union.
Mchezaji bora wa ligi kuu msimu uliopita, Muivory Coast, Kipre Tchetche ambaye alikosekana katika michezo ya vichapo kutoka kwa JKT Ruvu na Ndanda FC, alifunga bao la kuongoza kwa timu yake katika dakika ya 84 akimalizia pasi ya chipukizi, Mudathir Yahya.
Mlinzi Shimari Kapombe alifunga bao lake la kwanza katika ligi kuu tangu alipojiunga na Azam. Kapombe alifunga bao la pili katika dakika ya 88 baada ya kupanda na mpira kutoka katikati ya uwanja. Coastal ilipata bao la kufutia machozi katika dakika ya mwisho ya mchezo kupitia kwa Mkenya, Ramadhani Salima mbaye amefikisha bao la nne msimu huu. Kwa matokeo hayo, Azam imepanda hadi katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 13 sawa na Yanga walio katika nafasi ya tatu.
Coastal imeshuka hadi katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 11. Mechi kati ya vinara wa ligi hiyo Mtibwa Sugar na Kagera Sugar iliyokuwa ipigwe katika uwanja wa Manungu ilivunjika mara baada ya kip;indi cha kwanza na Mtibwa ilikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Ahmed Ally.
Mchezo huo utachezwa tena siku ya kesho. Mbeya City wameendelea kuchezea vipigo baada ya leo hii kutandikwa bao 1-0 na Stand United katika uwanja wa Kambarage. City wamepoteza mchezo wa tano msimu huu hivyo kuzua wasiwasi mkubwa wa kibarua cha kocha Juma Mwambusi.
Katika mchezo wa Polisi Morogoro na Tanzania Prisons katika uwanja wa Jamhuri, wenyeji Polisi wamefanikiwa kushinda kwa mara ya pili mfululizo baada ya wiki iliyopita kuifunga JKT Ruvu. Polisi imeshinda bao 1-0.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment