TANTRADE NA TAASISI YA GLOBAL EDUCATION LINK LTD KUFANYA MAONESHO YA ELIMU DESEMBA 10-14-2014 JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mkuu wa Tan Trade,  Jacqueline Maleko.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacqueline Maleko (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Maonesho ya Kwanza ya Kimataifa ya Elimu yatakayofanyika kuanzia Desemba 10 hadi 14, 2014 katika Uwanja wa  Maonesho wa Mwalimu JK. Nyerere Barabara ya Kilwa. Maonesho hayo yanafanywa na TanTrade kwa kushirikiana na Taasisi ya Global Education Link Ltd. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara za Ndani Tanzania, Edwin Rutageruka na Mkuu wa Taasisi ya Global Education Link Ltd, Abdulmalic Mollel. 
 Wanahabari wakichukua taarifa kuhusu maonesho hayo.
Wanahabari wakichukua taarifa kuhusu maonesho hayo.

Dotto Mwaibale

WASHIRIKI zaidi ya 500 na watembeleaji 350,000 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki katika maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya elimu nchini (TIEE).

Akizungumza Dar es Salaam leo,  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Global Education Link Ltd  Abdulmalik Mollel alisema, maonyesho hayo yanaandaliwa na kuratibiwa na taasisi yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade).

Alisema lengo kuu la maonesho hayo ni kuwatambulisha wadau wote wa masuala wa elimu ili kuweza kutoa huduma kwa wananchi kwa pamoja na kuwaelimisha juu ya mambo muhimu yaliyopo katika kila sekta.

"Maonesho haya yataleta manufaa makubwa na changamoto chanya hasa katika kuongeza ushindani kwenye sekta ya elimu ambayo itasaidia mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN)," alisema.

Mollel alisema baadhi ya faida za kushiriki maonyesho hayo ni kutengeneza ushindani wa bidhaa ya elimu katika sekta hiyo pamoja na wananchi kupata fursa ya kuchagua kozi na kuzielewa kabla ya kufanya maamuzi yao ya mwisho.

Aidha Mollel alisema maonyesho hayo yatawalenga wanafunzi wote kuanzia ngazi ya shule ya msingi, sekondari pamoja na wanafunzi kutoka katika vyuo mbalimbali vilivyopo hapa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tan Trade,  Jacqueline Maleko alisema ili kuweza kufanya vizuri katika mambo mbalimbali yanayohusu biashara ni lazima kuwa na elimu ya kutosha, hivyo maonyesho hayo yatawasaidia wanafunzi kupata elimu bora itakayowasaidia kufanya biashara zao kwa umakini.

"Kama sekta ya elimu atutaijengea mazingira mazuri, hapo baadae tutapata mafarakano makubwa kwani tutakuwa na wimbi kuwa la watu ambao awajasoma na iweleweke kuwa mataifa wenzetu wanapata nafasi mablimbali za kazi kwa sababu wanajitanza lakini sisi tunavyo vyuo vikubwa na vizuri tunashindwa kuvitangaza." alisema.

Hata hivyo Maleko amewataka wanafunzi pamoja na wazazi kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo ambayo yataanza rasmi tarehe 10 hadi 14 desemba katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam. 

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment